Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) anakaribisha maombi ya kujiunga na Chuo katika kampasi ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya kwa masomo yatakayoanza mwezi Machi katika ngazi za Astashahada (certificate) Stashahada (Diploma) kwa ajili ya muhula wa masomo wa 2021/2022.
CHUO KINATOA ASTASHAHADA (CERTIFICATE) NA STASHAHADA (DIPLOMA) KATIKA FANI ZIFUATAZO:
- Uhasibu (Accountancy)
- Masoko (Marketing Management)
- Usimamizi wa Biashara (Business Administration)
- Manunuzi na Ugavi (Procurement and Supplies Management)
- Vipimo na Mizani (Metrology and Standardization) na
- TEHAMA (Information Technology)
SIFA ZA KUJIUNGA:-
- Astashahada (Certificate), muombaji awe amemaliza kidato cha nne, mwenye ufaulu wa angalau alama “D” nne, au mwenye NVA level 3.
- Stashahada (Diploma), muombaji awe amemaliza kidato cha sita, mwenye ufaulu wa angalau alama “E” (Principal pasi moja) na “S” (Subsidiary pasi moja), Au awe amefuzu ngazi ya cheti katika chuo kinachotambulika na NACTE.
Gharama za maombi ya kujiunga ni shilingi 10,000/= tu. Ada zetu ni nafuu na zinalipwa kwa awamu. Ukipata ujumbe huu mjulishe na mwenzako, wahi mapema ili usipoteze fursa hii muhimu.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia, barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. au piga simu: DSM 0655 250 115/ Dodoma 0767 097 463/ Mwanza 0763 296 874/ Mbeya 0652 255 633.
BONYEZA HAPA KUTUMA MAOMBI